Na YASSIR MKUBWA EL BAHSAANY
Vijana wa kike nchini wametakiwa kuchangamkia fursa zinazotolewa na sekta binafsi ambazo zitawasaidia kuwapatia fursa za kiuchumi pamoja na kujiendeleza kimaendeleo.
Hayo yameelezwa na Mhifadhi wa mazingira ya bahari kisiwa cha chumbe Khamis Khalfan katika sherehe ya kuwapongeza wahitimu wa mafunzo ya urenja huko katika kituo cha walimu kiembe samaki wilaya ya magharibi B mkoa wa mjini magharibi Unguja
Amesema vijana wana nafasi ya kushiriki katika mambo mbali mbali yanayohusu uhifadhi wa mazingira hasa ya bahari ndipo uongozi wa chumbe ukaamuwa kutangaza nafasi kwa vijana ambao watataka kushiriki kwenye mafunzo hayo ya uhifadhi wa bahari
Aidha ameeleza kuwa vijana ambao wamepata nafasi ya kushiriki mafunzo hayo wanarajia kuwa marenja wazuri baada ya kumaliza mafunzo yao ikiwemo kutowa elimu kwa jamii juu ya kutunza mazingira ya bahari na viumbe vya baharini
Kwa upande wake Salim Abdallah Salim kutoka Kitengo cha Uhifadhi na elimu chumbe Island amewapongeza vijana hao kwa nafasi walioipata ya ushiriki wa mafunzo ya urenja hivyo amewataka kuendeleza elimu walioipata ya uhifdhi wa mazingira pamoja na kuwapatia vijana wengine.
Aidha amesema chumbe island inatowa mafunzo ya uhifadhi wa mazingira kwa vijana mbali mbali pamoja na kuwafundisha namna ya kuogelea na kufanya doria za bahari.
Pamoja na hayo amefahamisha kuwa chumbe island wanaendelea na utwaji wa elimu kwa watu mbali mbali na kuwataka vijana wachangamkie fursa ambazo zinatolewa hapoo
Msimaizi wa urenja kwa upande wa wanawake bi Magret Msemakweli Ntongwa amewahimiza vijana wa kike kujitokeza kwa wingi kwenye mafunzo ambayo yanatulewa chumbe katika nafasi ya urenja hivyo amewataka wale ambao wamepatiwa nafasi hiyo kuwashajihisha wengine kujitokeza pale ambapo nafasi zitatolewa.
Nao washiriki wa mafunzo ya urenja wametowa pongezi kwa chumbe island kwa kuona ipo haja kwa vijana wa kike kupewa nafasi ya kushiriki katika uhifadhi wa mazingira na rasilimali za bahari kutokana na nafasi hizo kushikiliwa na wanawake
Jumla ya vijana kumi wa kike wamepatiwa mafunzo ya urenja pamoja na uhifadhi wa mazingira ya bahari pamoja na matumbawe na kufanya doria za usalama bahari na kupatiwa vyeti vya ushiriki pamoja na vijana wawili kupata nafasi ya kuendelea kujifunza zaid kwa muda wa miezi mitatu.
MWISHO.