NA MUANDISHI WETU
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amehudhuria katika Hafla ya Hauli ya kumuombea dua Alhabib Sheikh Ahmad bin Aboubakar bin Sumeit anaetimiza miaka 102 tokea kufariki kwake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaomba wananchi kuendelea kushikamana, kuwa wamoja, kudumisha amani na utulivu ili kuzidi kupiga hatua ya maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii nchini.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Dua ya kumuombea Mwanachuoni mkubwa Zanzibar Alhabyb Ahmad Bin Abuubakar Bin Sumeit iliyofanyika Msikiti wa Ijumaa Malindi , Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 22 Aprili 2024.
Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa leo imemitimia miaka 102 tangu kufariki kwa Mwanachuoni Alhabyb Ahmad Bin Abuubakar Bin Sumeit amemuombea kwa Mwenyezi Mungu amrehemu na Wanazuoni wengine.
Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi ameishukuru na kuipongeza Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar kwa kuendelea kuratibu shughuli za Dini na kuzisimamia.
Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amesema jukumu la kuwaombea Dua Waislamu waliotangulia ni la kila Muumini wa Dini hiyo.
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume na Sheikh Mudhihiriddiyn Ally Qulateyn wakamuelezea Sheikh Alhabib Ahmad bin Aboubakar bin Sumeit katika harakati zake za dini na mazingira ya kuishi na jamii
Hauli hio ya Sheikh Ahmad bin Sumeit imeandaliwa kwa pamoja baina ya uongozi wa Msikiti Gofu na Msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi.
MWISHO.
KABURI HILO LIPO MBELE YA MSIKITI WA IJUMAA MALINDI ALIPOSHIRIKI KATIKA HAULI YA KUTIMIZA MIAKA 102 TOKEA KUFARIKI KWAKE.