Tuesday, 9 May 2023

ZAIDI YA MITI 5000 YA ASILI NA MATUNDA INATARAJIWA KUPANDWA MATEMWE

NA THABIT MADAI, ZANZIBAR 

KATIKA Kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Tabia Nchi, Jumla ya Miti 5000 inatarajiwa kupandwa katika Kijiji cha Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja kupitia Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mfumo wa Ikolojia Vijijini (EBARR).

Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mfumo wa Ikolojia Vijijini unatekelezwa katika ya Simanjiro, Mpwapwa,Mvomero, kishapu na Wilaya ya Kaskazini A Unguja.

Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari huko Maruhubi Mjini Magharib Unguja, Mratibu wa Mradi wa EBARR  wa Zanzibar, Alawi Haji Hija, alisema kuwa lengo la upandaji wa Miti hiyo ya Asili na Matunda ni lengo la kuhimili mabadilko ya tabianchi na kurejesha uoto asili na matumizi bora ya ardhi.

Pia alisema, kupitia mradi huo pia watajenga vitalu nyumba ambapo ni kilimo kimekuwa kikistahamili ukame.

Alisema,mradi huo kwa upande wa Zanzibar wanatekeleza kwa shehia tatu zilizoko katika kijiji cha Matemwe, ikiwemo shehia ya Matembe kijini, Matemwe mbuyu tende na shehia ya Matemwe Jugakuu.

Alisema, lengo la mradi huo ni kuimarisha uoto wa asili kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi, ambapo alisema athari hizo zipo katika maeneo mbalimbali na kila eneo limekuwa na athari zake.

“Kwa upande wa matemwe ni maeneo ambayo yameathirika na kunatatizo kubwa la ukosefu wa mvua za kutosha na ukiangalia katika mazingira ya eneo lile kuna uharibifu mkubwa wa misitu” alisema.

Hivyo, alisema wataendeleo kurejesha hali hiyo sambamba na kuwapatia kipato wananchi kwa kuwawezesha kupata kipato chao bila ya hata kuharibu mazingira.

Hivyo, alisema mradi huo umekuwa unawasaidia wanajamii hata kupata kipato na kuwahimiza shughuli zao zisiwe moja kwa moja atika shughuli za kuharribu mazingira.

Alisema ili kudhibiti suala hilo, wamegenga majiko banifu ambapo yamekuwa yakitumia kuni chache kwa muda mrefu, jambo ambalo limekuwa likiwapa afueni miti iliyozunguka katika eneo hilo.

Aidha alisema pia kupitia mradi huo wamechimba visima sita vimechimbwa ili kuwezesha upatikanaji wa maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kilimo cha mbogamboga, wameviwezesha vikundi vya uvuvi kwa kuwanunulia boti sita za kisasa.

Nao, waandishi wa habari, wamesema watendelea kushirikiana na watendaji wa mradi huo ili kuona hali ya tabiachi inaendelea kuimarika sambamba na kuahidi kutoa elimu kwa jamii ili kuondokana na uharibifu wa mazingira.

Mradi wa EBARR unatekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Shirika La Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP)ambapo utekelezaji huo ulianza mwaka 2018 na unategemewa kukamilika Februari  2024.

MWISHO.



Wednesday, 3 May 2023

UHURU WA HABARI UTUMIKE KATIKA KUJIELEZA

Na Muandishi Wetu 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa wito kwa tasnia ya habari kuitumia fursa ya maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kuweka mkazo mkubwa kwenye uhuru wa kujieleza ndani ya ajenda ya jumla ya haki za binaadamu, kwa kuangazia uhusiano baina ya uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza na haki nyengine.

Aidha, aliwaasa waandishi wa Habari kushirikisha wahusika wote kwa madhumuni ya kulinda uhuru wa vyombo hivyo, kuimarisha uhuru wa kujieleza, na kuweka mazingatio ya haki za binaadamu kama ni kitovu cha kufanya maamuzi katika ngazi ya kimataifa, kikanda na kitaifa.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani huko ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa ndege, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Katika maadhimisho hayo, Rais Dk. Mwinyi pia aliwataka waandishi wa habari kutimiza ahadi zilizotolewa na kila nchi Mwanachama wa Umoja wa Mataifa ili kuyafikia malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).

Pia Dk. Mwinyi aliwataka wadau wa vyombo vya habari kuitumia siku hiyo kusherehekea kwa kuungana na mashirika yanayotangaza masuala ya mazingira, haki za wanawake, watoto, haki za kiasili, haki za kidijitali, vita dhidi ya ufisadi na mengineyo.

Alisema, maadhimisho hayo ni jukwaa muhimu katika kuibua changamoto za kisera na kuangalia namna bora ya kuboresha mazingira ya kuendesha vyombo vya habari nchini.

Akizungumzia sheria ya Habari, Rais Dk. Mwinyi alisema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari imeandaa mswada wa sheria hiyo yenye madhumuni ya kufuta Sheria iliyopo ya Usajili wa Magazeti, Wakala wa Habari na vitabu Sheiria nambari 5 ya mwaka 1988 ambapo marekebisho yake ni sheria nambari 8 ya mwaka 1997 na kutunga Sheria mpya ya Huduma za Habari na Mambo yanayohusiana na hayo.

Dk. Mwinyi alieleza kwamba Mswada huo tayari uko Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na unatarajiwa kutoa sheria nzuri itakayohusiana na masuala ya habari.

Alisema Zanzibar, imekuwa na kasi ya usajili mpya wa vyombo vya habari hasa vya kielektroniki kupitia Tume ya Utangazaji baina yam waka 2020 hadi 2023. Kwa mijibu wa tume hiyo Dk. Mwinyi alieleza jumla ya TV 21 za kawaida na 38 za mitandaoni zimesajiliwa, jumla ya redio 27 zikiwemo za masafa ya FM na za jamii zimesajiliwa. 

Aidha, alizungummzia Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, magazeti na majarida 71 yamesajiliwa tangu mwaka 1998 hadi 2023. Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) na Shirika la Magazeti ya Serikali ni vyombo vya habari vya Serikali ambavyo navyo vimekuwa vikifanya kazi kubwa za kutoa taarifa kwa umma.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Andrew Kundo, aliviasa vyombo vya Habari nchini kufanyakazi kwa kuzingatia, miongozo, kanuni na sheria zilipo katika utekelezaji wa majukumu yao.

Naye, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita, alisema Serikali kupitia Wizara ya Habari itaendelea kushirikiana na wadau wa vyombo vya Habari nchini ili kuendelea kuwapasha habari wananchi.

Mkurugenzi kutoka Chama Cha Waandishi wa Habari wanawake Tanzania, TAMWA, Joyce Shebe aliomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuharakisha mchakato wa Sheria ya Habari.

Jumla ya magazeti 312 yalisajiliwa nchini hadi tarehe 20 Februari, mwaka huu, ambapo baada ya Uhuru wa Tanganyika, kulikuwa na magezeti 10 tu.

Kwamujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) hadi mwezi Februari mwaka huu, jumla ya redio 218, televisheni 68, redio za mtandao nane, televisheni za mtandao 391, blog, majukwaa 73 na cable operators 53 zimesajiliwa Tanzania bara, ambapo taarifa za baada ya uhuru zinaonyesha tulikuwa na kituo kimoja tu cha redio cha Tanganyika na hakukuwa na kituo cha televisheni hata kimoja, blogs wala majukwaa ya mtandaoni.




UJENZI WA VITUO VYA MABASI KUTAONDOSHA CHANGAMOTO KWA WANANCHI

 UJENZI WA VITUO VYA MABASI KUTAONDOSHA CHANGAMOTO KWA WANANCHI

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dk. Khalid Salum Mohamed ameitaka kampuni ya CRJE Tanzania iliopewa kazi ya kujenga kituo cha mabasi katika eneo la kijangwani kuhakikisha wanazingatia viwango na kukamilisha mradi huo ndani ya wakati uliopangwa.

Waziri Dk. Khalid ametoa agizo hilo wakati aliposhiriki na kushuhudia zoezi la utiaji saini wa ujenzi wa kituo hicho hafla iliofanyika katika ukumbi wa ZSSF Kariakoo.

Zoezi la utiaji saini kwa upande wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF) imewakilishwa na Mkurugenzi Muendeshaji wa Mfuko huo ndugu Nassor Shaaban Ameir na kwa upande wa Kampuni ya CRJE imewakilishwa na meneja wao XU CHANG.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi la utiaji saini Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dk. Khalid Salum Mohamed ameupongeza uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF) kwa uthubutu pamoja na ubunifu wao wa kutekeleza miradi ya maendeleo.

Aidha, Mhe. Waziri ameutaka uongozi wa ZSSF kuhakikisha wanasimamia kwa karibu ujenzi wa kituo hicho kwa kuteua mshauri elekezi ataekasimamia kwa upande wa Serikali na kuhakikisha ujenzi huo unakamilishwa kwa viwango vinavotakiwa.

Pamoja na mambo mengine Waziri Dk. Khalid amesema ZSSF inakwenda kurejesha historia kwa kukijenga kituo cha mabasi katika eneo hilo kwani mnamo miaka ya 1970 eneo hilo lilikua likitumiwa kwa shughuli kama hizo.

Pia, Mhe. Waziri amepongeza ushirikiano mzuri ulitolewa na askari wa UMAWA kwa kukubali kupisha ujenzi wa kituo hicho na kuhamishia Afisi zao katika eneo jengine lililotolewa na Serikali.

Nae Mkurugenzi Muendeshaji wa mfuko wa Hifadhi ya Jamii Ndugu Nassor Shaaban Ameir amesema ZSSF imeamua kujikita katika ujenzi wa vituo vitatu vya mabasi kwa hatua ya awali lengo likiwa ni kutatua changamoto na kuwaondoshea usumbufu wananchi katika huduma ya usafiri.

Amebainisha vituo hivyo vitajengwa katika eneo la Kijangwani, Malindi pamoja na katika eneo la Mnazi mmoja huku wakisogeza huduma ya ujenzi wa vituo hivyo nje ya mji kulingana na uhitaji.

Vile vile Mkurugenzi Nassor amemuomba Mhe. Waziri kupitia wizara anayoisimamia kuziagiza mamlaka za usafiri pamoja na mabaraza ya manispaa na mabaraza ya miji kuanza kutunga kanuni na kuandaa utaratibu wa kutumika kwa vituo hivyo mara vitakapokamilika.

Kwa upande wake Meneja wa kampuni ya CRJE Tanzania XU CHANG ameeleza kwamba, kampuni yao itahakikisha inajenga kituo hicho katika ubora unaotakiwa na kumaliza kwa wakati uliopangwa ambapo wanakusudia kuingiza vifaa vya ujenzi vya kisasa katika kutekeleza kazi hiyo ya ujenzi.

Ujenzi wa Kituo hicho unatarajiwa kugharimu jumla ya Shilling Billlioni nane milioni mia sita nasabiini, laki nne na arubaini na tisa mia tatu ishirini na moja nukata mbili moja (8,670,449,321.21) na kinakadiriwa kuwa na maduka sabiini na nane (78), sehemu za kupata huduma kutolea fedha sita, sehemu za kutoa huduma za chakula tano pamoja na huduma za vyoo ambapo ujenzi wake utachukua miezi kumi (10) hadi kukamilika kwake. 




Monday, 1 May 2023

WANNE MIKONONI MWA POLISI KWA WIZI WA HONDA

 NA MUANDISHI WETU - ZANZIBAR

JESHI LA POLISI MKOA WA KUSINI UNGUJA LIMEWAKAMATA WATU WANNE

WAKIWA NA PIKIPIKI MBILI ZINAZODAIWA KUWA NI ZA WIZI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA KUSINI UNGUJA, KAMISHNA MSAIDIZI WA

POLISI ACP GAUDIANUS KAMUGISHA AMEWATAJA WATUHUMIWA HAO KUWA NI

MOSES EDWIN ENDRU MIAKA 28 NA AHMADA MSHAMBA MUSSA MIAKA 27

WOTE WAKAAZI WA MWERA, WILAYA YA MAGHARIBI ”A” WAMEPATIKANA

WAKIWA NA PIKIPIKI MOJA AINA YA TVS RANGI NYEUSI YENYE NAMBA ZA USAJILI

Z.944 KU AMBAYO INADAIWA KUIBIWA MAENEO YA TUNGUU.

AIDHA KAMANDA KAMUGISHA AMEWATAJA ABDUL-RAHMAN SULEIMAN SAID

MIAKA 32 NA ALI ABDALLAH ABDALLAH MIAKA 48 WOTE WAKAAZI MIGOMBANI

MJINI UNGUJA WAKIWA NA PIKIPIKI MOJA RANGI NYEUSI AINA YA TVS YENYE

NAMBA ZA USAJILI MC.884 CKZ.