Na Yassir Mkubwa EL BAHSAANY
Wadau wa kupinga Vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji wa kijinsia wamesema Sheria ya Mtoto namba 6 ya mwaka 2011 ni vyema ikatambua mgawanyo wa haki za watoto kwa kuzingatia umri ili kulinda maslahi na ustawi wa mtoto.
Wito huo umetolewa na na Hakimu dhamana Mkoa wa Kusini Unguja ndugu Khamis Rashid Khamis Mara baada ya kikao cha Mapitio cha kujadili sheria ya Mtoto na kutoa maoni kilichofanyika katika ukumbi wa kidongo chekundu Mental.
Amesema ni wakati sahihi wa kueka sheria ambayo Itatoa muongozo wa kushughulikia watoto wenye umri wa chini ya miaka 14 na 16 na kuweka utaratibu wa kusikiliza kesi zao.
Hata hivyo amependekeza suala la kueka sheria kwa skuli zinazolea watoto kuhakisha wanaimarisha mfumo wa kuieka saikolijia ya mtoto mhanga wa matukio mbali mbali nchini.
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto ndugu Siti Abas Ali amesema umuhimu wa marekebisho ya Sheria ya mtoto ni pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia ambayo kimsingi yameongeza haja ya kuimarisha baadhi ya vipengele vyake.
Aidha Mkurugenzi Siti amesisitiza suala la ushirikiano na wadau mbali mbali katika katika mapambano ya ukiukwaji wa haki za mtoto.
Amesema Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ipo tayari kushirikiana na wadau hao ili kufanikisha azma ya kuleta ustawi wa mtoto.
Baadhi ya wanasheria wamesema kikao hicho ni miongoni mwa sheria yoyote ni kutekeleza hivyo uwepo wa Ushirikishwaji wa wadau hao utasaidia kuleta ufanisi wa kiutekekelezaji wa sheria hiyo.
Wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia Wazee na watoto inaendelea na ukusanyaji wa maoni ya sheria ya hiyo kwa lengo la kuipata sheria mpya na iweze kudumu kwa muda mrefu.
MWISHO
No comments:
Post a Comment