Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud amesema serikali inaendelea kushirikiana na sekta binafsi ili kuona changamoto zinazozikabili sekta mbalimbali ikiwemo elimu zinapatiwa ufumbuzi.
Akizungumza katika hafla ya ugawaji wa vifaa vya elimu kwa wanafunzi wa skuli ya Mgonjoni vilivyotolewa naTaasisi ya Bhoke Moren Foundation amesema kutolewa kwa vifaa hivyo vitawasaidia wanafunzi hao kusoma katika mazingira mazuri.
Amesema matumaini yake kuwa taasisi hiyo inakuwa mkombozi wa wanafunzi ktk sekta ya elimu hapa zanzibar .Amesema serikali imefanya juhudi za kutosha kuhakikisha kijiji cha mgonjon kinapata mafanikio pamoja na kupatiwa huduma zote za msingi ikiwemo elimu na huduma nyengine za kijamii.
Mwenyekiti wa Bhoke Moroni Foundation Bhoke Moroni amesema taasisi ya Bhoke amelenga kusaidia watoto wenye kuishi katika mazingira magumu hivyo atahakikisha misaada yote inayotolewa inawafikia walengwa ili kuwaondolea changamoto mbalimbali ikiwemo kwenye elimu. Ameeleza lengo ni kuinua ufaulu wa wanafunzi wenye kuishi katika mazingira magumu wakiwemo watoto yatima amesema katika kuangalia mazingira wamegundua mazingira hatarisi ikiwemo viatu na sare za skuli.
Ameahidi kuwapatia wanafunzi viatu na sare za skuli ili kuondoa tatizo hilo ambalo wanafunzi wengi wanakabiliwa nalo kutokana na ugumu wa maisha katika familia zao.
Akisoma Risala ya walimu ya Skuli ya Mgongoni Mwalimu Zainab Sururu Vuai amesema Skuli ya Mgonjon bado inakabiliwa na changamoto ya Uzio wa skuli, Usafiri kwa walimu, ukosefu wa uwanja wa michezo, walimu wa masomo ya Sayansi komputa na ICT.Hivyo ameiyomba serikali kupitia wizara ya elimu kuongeza bajeti ili kujiendesha kwa ufanisi katika kukuza ufaulu kwa wanafunzi wa skuli hiyo.
Hata hivyo waliishukuru taasisi ya msaada Bhoke Moroni Foundation kwa kuwapatia msaada hu wa vifaa na kuahidi kuvitumia kwa lengo lililokusudiwa na taaasisi hiyo. Nao wanafunzi waliokabidhiwa msaada huo wamatoa shukurani zao za dhati kwa taasisi ya Bhoke ambao utawasaidia katika masomo yao.