Friday, 1 November 2024

Uhispania yaomboleza huku idadi ya vifo vya watu waliofariki kutokana na mafuriko ikizidi 150

 Uhispania yaomboleza huku idadi ya vifo vya watu waliofariki kutokana na mafuriko ikizidi 150

Takriban watu 158 wamefariki katika maafa makubwa zaidi ya mafuriko nchini Uhispania katika vizazi huku waokoaji wakipambana kutafuta manusura.
Siku ya Alhamisi zaidi ya wafanyakazi 1,200, wakisaidiwa na ndege zisizo na rubani, wametumwa kufanya kazi ya uokoaji huku mvua ikiendelea kusababisha tisho la maafa zaidi maeneo mbali mbali ya nchi hiyo.
Lakini katika baadhi ya miji iliyoathiriwa zaidi na mafuriko ya Jumanne usiku, watu walikumbwa na kazi ya kuopoa miili kutoka kwenye matope na vifusi vya majengo yaliyoporomoka kufuatia mafuriko.
Vifo visivyopungua 155 vilirekodiwa katika mji wa Valencia, huku vingine viwili vikirekodiwa katika eneo la Castilla-La Mancha magharibi mwa jimbo hilo, na raia Muingereza, ametangazwa kufariki Andalusia.



No comments:

Post a Comment