Sunday, 24 November 2024

TAMWA YATOWA MAFUNZO KWA WAHAMASISHAJI JAMII KUHUSU MAFUNZO YA NAFASI ZA UONGOZI KWA WANAWAKE

 




Na Muandishi wetu.

Katika juhudi za kuimarisha ushiriki wa wanawake katika uongozi na kukuza haki za kidemokrasia, Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA- ZNZ) kimetoa mafunzo ya siku mbili kwa Wahamasishaji Jamii (Citizen Brigades) wapatao 60 kwa upande wa Unguja ikiwa ni sehemu ya program ya kuimarisha uongozi kwa wanawake (SWIL) wenye lengo la kujenga jamii yenye usawa wa kijinsia kwa kuwawezesha wanawake kushika nafasi katika ngazi za maamuzi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano TAMWA ZNZ, Saphia Ngalapi, ameeleza kuwa watekelezaji wa program wanaimani na wahamasishaji waliopatiwa mafunzo na kuwawata kuwa mabingwa wakuhamasisha jamii juu ya haki za wanawake kushiriki katika uongozi.

"Kupitiatimuhii, tunatarajia mabadiliko katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu haki ya demokrasia na uongozi kwa wanawake ili kufikia 50% kwa 50% katika ngazi za maamuzi, jambo litakalochangia kuleta maendeleo endelevu kwawote" alisema Ngalapi.

Afisa Ufuatiliaji na Tathmini TAMWA ZNZ, Mohamed Khatib, aliwasisitizia wahamasishaji hao juu ya umuhimu wa kazi yao katika kukuza nafasi za wanawake katika uongozi.

"Tufahamu kuwa hili jambo la kuelimisha jamii si ajira bali ni kazi yakujitolea kuhakikisha matarajio ya wanawake kushika nafasi za uongozi yanafikiwa kwa kubadilisha mitazamo ya jamii, uchaguzi wa 2025, tunataka tuone wanawake wanashika nafasi za uongozi kuanzia ngazi za shina hadi Taifa kwani uwezo huo wanao, alifafanua afisa huyo.





Mafunzo haya yamejumuisha wawakilishi kutoka makundi mbali mbali ya kijamii ikiwemo viongozi wa dini, watu wenye ulemavu, wanaharakati wa kupinga vitendo vya udhalilishaji na wanaume wa mabadiliko.

Nae mkufunzi ni mafunzo hayo ya siku mbili Asha Abdi aliwahimiza wahamasishaji jamii kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha malengo ya mradi huu yanafikiwa.

Ukhty Amina Salum ambae ni kiongozi wa dini na mwanaharakati wa siku nyingi ameeleza shukrani zake kwa kuchaguliwa kuwa sehemu ya wahamasishaji wa jamii. "Nafurahi kuwa miongoni mwa wahamasishaji wa jamii, dhamana hii nitaibeba na kuhakikisha jamii inahamasika na kuachana na dhana potofu juu ya uwezo wa mwanamke na maamrisho ya dini kuhusiana na wanawake kushiriki katika uongozi alisema Ukhty Amina.

Nae Haji Khamis Haji kutoka Mkoa wa Kaskazini Unguja alisisitiza kuwa elimu aliyoipata itamsaidia kuhamasisha jamii katika mkoa wake kutambua haki zao za kidemokrasia na kuongeza wanawake katika nafasi za uongozi.

Mafunzo haya yanaashiria jitihada za TAMWA- ZNZ kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wanawake Wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA), Jumuiya ya Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO) Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) kwa mashirikiano makubwana Ubalozi wa Norway katika kuwaandaa wanawake wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi kuelekea uchaguzi wa 2025, huku wakilenga kuongeza idadi ya wanawake katika ngazi za maamuzi visiwani Zanzibar.










Saturday, 23 November 2024

WANANCHI WAPIMWA AFYA ZAO BURE KUELEKEA KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA UVUVI

 




Na Seif Mbarouk - Malindi

Wavuvi mbali mbali wametakiwa kuunga mkono shamrashamra za wiki ya uvuvi katika ukataji wa leseni za uvuvi ili kuachana na uvuvi haramu unaoendelea kufanyika siku hadi siku.

Amesema hayo Meneja wa Diko na Soko la Samaki la Malindi Nd. Mohd Idarus Mohd wakati wa ufanyaji wa usafi wa soko la samaki pamoja na upimaji wa afya kwa wananchi huko Malindi Mkoa wa Mjini Unguja.

Meneja huyo amesema miongoni mwa shamrashamra za wiki ya mvuvi ni kuwahamasisha wavuvi kufuata sharia za uvuvi ikiwemo ukataji wa leseni kwa ajili ya kuimarisha shughuli za uchumi wa buluu nchini.

Sambamba na hayo amesema lengo la kuadhimisha siku ya Mvuvi Duniani nu kujadili mambo mbali mbali yanayohusiana na uvuvi ili kutambua umuhimu wa sekta ya uvuvi pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo.

Kwa upande wake Mratibu wa Kifua Kikuu Zanzibar Dkt. Rahma Omar kutoka Shirika la Amred Tanzania amesema lengo la kuendesha shughuli za afya katika Soko la Malindi ni kuwasogezea huduma kwa karibu ili kuwakinga na hatari ya kupata ugonjwa wa kifua kikuu.

Vilevile amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imegharamia huduma za afya kwa wananchi hivyo wananchi mbalimbali wanapaswa kujitokeza kwa wingi kupata huduma mbalimbali kama upimaji wa shindikizo la damu ,homa ya ini ,kisukari na mengineo.

Kwa upande wao Washiriki wa zoezi hilo wamesema wameishukuru Serikali kwa kuadhimisha siku ya Mvuvi Duniani kwa kuwaletea huduma ya afya bure na kutoa wito kwa wavuvi wa diko la Malindi kuja kushiriki zoezi hili ili kuwa na uhakika wa afya zao.

MWISHO.


Wednesday, 20 November 2024

MTU MMOJA MIKONONI MWA POLISI AKITUHUMIWA KUBAKA NA KUSABABISHA KIFO CHA MTOTO WA MIAKA SITA

 MTU MMOJA MIKONONI MWA POLISI AKITUHUMIWA KUBAKA NA KUSABABISHA KIFO CHA MTOTO WA MIAKA SITA





Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja linamshikilia mtu mmoja aitwae Maulid Hassan Maulid (18) mkaazi wa Mwera Pongwe katika Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja kwa tuhuma za mauaji ya mtoto mdogo Khadija Dadi Mhoda (06) mwanafunzi wa chekechea mkaazi wa Mwera Vichaka mabundi, shehia ya ubago.
Akizungumza na waandishi wa habari huko Tunguu , Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Kusini unguja, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Daniel Shillah amesema tukio hilo la Mauaji lilitokea Novemba 14, 2024 huko Mwera Vichaka Mabundi ambapo Mtuhumiwa huyo alimwingilia kimwili na kumsababishia kifo chake.
Kamanda SHILLAH amesema Jeshi la Polisi Katika Mkoa huo linaendelea kufanya upelelezi ili mtuhumiwa huyo afikishwe Mahakamani.

AJALI ZINAWEZA KUEPUKIKA KWA MADEREVA IKIWA WATAKWENDA MWENDO WA WASTANI


Na Muandishi wetu

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Rashid Hadid Rashid, amewataka madereva kwenda mwendo wa wastani wakati wanapoendesha vyombo vya moto ili kuepuka ajali zisizo za lazima.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu huyo, wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuendesha kwa usalama, madereva na makonda wa gari za abiria wa mkoa huo, katika ukumbi wa Ofisi ya Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘B’, Othman Ali Maulid, amesema uzowefu unaonesha kuwa mwendo kasi unachangia ajali nyingi za barabarani na kuwataka wadau hao kufuata maelekezo ya mwendo yaliyowekwa katika alama za barabarani ili watumiaji wa barabara wabaki kuwa salama.
Ameeleza kuwa Serikali imeweka miundombinu ya barabara ili kuhakikisha sekta ya usafiri nchini inaimarika na kuwasihi kuitumia miundombinu hiyo kama ilivyokusudiwa pasi na kuathiri watumiaji.
"Tunapoendesha vyombo vyetu kwa mwendo wa wastani itasaidia kupunguza ajali na endapo zitatokea hzaitakua kubwa kama itavyokua ajali ya mwendo kasi.” alisema Mkuu huyo.
Aidha amewataka waliopatiwa mafunzo hayo kuwa mabalozi wazuri wa elimu hiyo ili kuiweka Zanzibar katika hali ya usalama kutokana na ajali za barabarani kwa Zanzibar bila ya ajali inawezekana.
Naye Mkuu wa Kituo cha Umahiri cha Kikanda katika Usalama Barabarani, Chuo Cha Taifa Cha Usafishaji (NIT ), Godlisten Msomanje amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhamasisha matumizi salama ya barabara katika kuadhimisha wiki ya usalama barabarani.
Alieleza kuwa chuo hicho kinatoa mafunzo kwa madereva, kufanya utafiti na kutoa ushauri elekezi ili kuhakikisha usalama wa wananchi barabarani unakuwepo muda wote.
Amesema uzowefu unaonesha kuwa tatizo la usalama barabarani ni janga la kitaifa hivyo elimu inahitajika zaidi ili kuondoa tatizo hilo
“tumekuja Zanzibar kutoa elimu dhidi ya usalama barabarani ili kusaidia kuweka usalama wa watumiaji wa barabara.” Alisema mkuu huyo
Akiwasilisha mada ya Sheria na alama za barabarani, Mhandisi Mhonja Roheje, amesema madereva wengi wanaenda kinyume na taratibu na sharia za barabarani ikiwa ni pamoja na kuendesha bila kuwa na leseni ya udereva, kutokagua vyombo vyao kabla ya kuingia barabarani pamoja na kutofuata alama za barabarani.
“Iwapo utakua na leseni lakini unajaza abiria kupitia kiasi bado hujafuata sheria jambo ambalo linahatarisha usalama wa abiria na watumiaji wengine wa barabara na kuiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kusimamia mikakati zaidi ili kukomesha tabia za madereva na makonda wanaofanya makosa hayo.”alisema Mhandisi huyo
Kwa upande wa madereva na makondawaliyopatiwa mafunzo hayo wameahidi kuyafanyia kazi kwa maslahi ya watumiai wa barabara na Taifa kwa ujumla na kuziomba taasisi husika kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara ili kutekeleza majukuumu yao kwa ufanisi.
Mafunzo hayo yametolewa na Mamlaka ya Usalama Barabarani Zanzibar kwa kushirikiana na Chuo Cha Usafirishaji Tanzania, ikiwa ni shamrashamra za wiki ya nenda kwa usalama Barabarani.








Friday, 1 November 2024

Vita vya Ukraine: Ndege 31 zisizo na rubani zimedunguliwa Ukraine, Jeshi la anga la Ukraine lasema

 Vita vya Ukraine: Ndege 31 zisizo na rubani zimedunguliwa Ukraine, Jeshi la anga la Ukraine lasema

kulingana na ripoti ya kila siku ya Ukraine kuhusu ya jeshi la anga la Ukraine, Usiku wa tarehe 1 Novemba, jeshi la Urusi limeishambulia Ukraine kwa makombora matatu ya ndege ya X-59/69, droni 48 za aina ya Shahed, pamoja na droni za "aina isiyojulikana,".
Pia inabainisha kuwa mfumo wa ulinzi wa anga, ulidungua droni 31 kwa risasi na droni nyingine 14 "zilipotea ndani," na tatu zaidi ziliruka kuelekea Belarus.
"Pia, ulinzi wa anga ulifanikiwa kuangusha kombora moja la ndege iliyokuwa ikiongozwa na droni ya X-59/69. Malengo ya mashambulizi ya Urusi hayakufikiwa,"
ripoti hiyo inasema,Jeshi la anga lilibaini kuwa, hakukuwa na majeruhi.
wizara ya ulinzi ya Urusi imesema,Urusi inaripoti kuwa jana usiku, mifumo ya ulinzi wa anga ilidungua ndege zisizo na rubani 83 za Ukraine katika maeneo ya Kursk, Voronezh, Bryansk, Oryol na Belgorod, pamoja na eneo lililotwaliwa na Urusi.



Uhispania yaomboleza huku idadi ya vifo vya watu waliofariki kutokana na mafuriko ikizidi 150

 Uhispania yaomboleza huku idadi ya vifo vya watu waliofariki kutokana na mafuriko ikizidi 150

Takriban watu 158 wamefariki katika maafa makubwa zaidi ya mafuriko nchini Uhispania katika vizazi huku waokoaji wakipambana kutafuta manusura.
Siku ya Alhamisi zaidi ya wafanyakazi 1,200, wakisaidiwa na ndege zisizo na rubani, wametumwa kufanya kazi ya uokoaji huku mvua ikiendelea kusababisha tisho la maafa zaidi maeneo mbali mbali ya nchi hiyo.
Lakini katika baadhi ya miji iliyoathiriwa zaidi na mafuriko ya Jumanne usiku, watu walikumbwa na kazi ya kuopoa miili kutoka kwenye matope na vifusi vya majengo yaliyoporomoka kufuatia mafuriko.
Vifo visivyopungua 155 vilirekodiwa katika mji wa Valencia, huku vingine viwili vikirekodiwa katika eneo la Castilla-La Mancha magharibi mwa jimbo hilo, na raia Muingereza, ametangazwa kufariki Andalusia.