Thursday, 23 November 2023

VODACOM TANZANIA WATOA BIMA KWA WATOTO 100 MNAZI MMOJA


NA YASSIR MKUBWA - ZANZIBAR TODAY

JUMLA ya mama 100 na watoto 100 wamepatiwa bima kubwa ya bure ya mwaka mzima na kampuni ya Teknologia na mawasiliano Vodadom Tanzania. 

Kina mama hao ni wale waliojifungua watoto wao kunazia Novemba 9 mwaka huu katika hospitali ya Rufaa Mnaznimmoja kupatiwa zawadi hiyo ya upendo. 

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi bima hizo Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Vodacom Tanzania, Anet Kanora, alisema hatua hiyo ni muendelezo wa kampuni hiyo kutoa zawadi kwa wateja wake ikiwa ni njia ya kuwashukuru lakini kwa mwaka huu wameona ipo haja ya kuifikia jamii pana ya watanzania.

Alisema afya ya mama na mtoto ni muhimu kwa kampuni hiyo hivyo wameona ipo haja ya kumpatia bima kubwa mama pamoja na mtoto wake itakayomuwezesha mama na mtoto wake kupata matibabu.

Aidha alisema kwa Tanzania nzima bima hiyo itanufaisha watoto 1000 na mama 1000 lakini kwa Zanzibar kinamama 100 na watoto 100 watanufaika na bima hiyo ya afya.
Alisema bima hizo zitatumika katika hospitali mbalimbali za Zanzibar ikiwemo Ampola Global, Tawakal, Alrahma na hospitali ya Rufaa Mnazimmoja kwa Zanzibar na hospitali ya Muimbili na nyengine za Tanzania bara.   

Mkuu Anet alibainisha kuwa bima hiyo itakuwa haina upendeleo kwani ni lazima watoto wote watakaozaliwa katika kipindi hichi basi wote watanufaika na bima hiyo kuona wanatibiwa magonjwa mbalimbali ikiwemo ya kulazwa ama kutibiwa na kuondoka.
Alibainisha kuwa anaamini bima hiyo itakwenda kuwasaidia wazazi na watoto wao kwani mwaka wa kwanza wa mtoto ni muhimu sana katika upimaji na upatikanaji wa afya bora katika makuzi ya mtoto.

Akizungumzia kuhusu kampeni ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’ Meneja Mauzo Vodacom Zanzibar, Fadhili Linga, alisema kampeni hiyo ina sehemu mbili, kwanza kuwazawadia wateja kwa zawadi mbalimbali na pili kujikita katika shughuli za kijamii.
Linga alisema sekta ya afya ni eneo muhimu na kampuni hiyo imeona iendeleze jitihada za kuunga mkono serikali kupitia miradi mbalimbali.

Aliahidi kuwa watanendeleza ushirikiano huo ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za matibabu ya afya kwa Watanzania wote zinapatikana bila ya usumbufu.
Alisema mbali na kutoa bima pia Vodacom imekuwa ikiwazawadia zawadi kama vile bodaboda, TV, simu za mkononi, router za 4G na 5G na pesa taslimu kuanzia shilingi 500,000 mpaka milioni 10,000,000.

Khadija Salum Said ni Mkuu wa Wodi ya Wazazi hospitali ya Rufaa Mmnazimmoja, aliipongeza kampuni hiyo kwa ubunifu wa kampeni hiyo ambayo inawajali kinamama wanaoleta viumbe wapya duniani.

Alisema kupatiwa bima hizo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa huduma ya uhakika ya afya katika hatua ya awali ya watoto wachanga na akina mama waliotoka kujifungua na kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga. 

Kwa kupatia bima ya afya ya bure, tena ile kubwa kwa mwaka mzima, akina mama hawa na watoto wao hawatokuwa na shaka pindi watakapokumbwa na changamoto za kiafya, ujio wenu huu umetusaidia sana kupunguza matatizo ambayo yatatokea baada ya mama kujifungua na hata kupunguza vifo vya watoto wachanga,”alisema.

Hivyo, aliiomba kampuni hiyo kuendelea kushirikiana pamoja katika mapambano ya kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa kusaidia bima hiyo kwa wazazi wa Tanzania nzima kwani utoaji wa bima hiyo ni njia moja ya kupunguza vifo hivyo. 

Wakizungumza kwa niaba ya wazazi wenzao waliopatiwa bima hizo Maryam Yohana Daniel na Badria Mohammed Khamis aliejifungua watoto mapacha walipongeza Vodacom kwa kuwapatia bima hizo ambazo zitawasaidia kupata matibabu wao na watoto wao na huduma nyengine za kiafya.

Hivyo waliiomba jamii kujiunga na kampuni ya Vodacom ili iweze kusaidia kundi kubwa zaidi katika jamii ya watanzania. 

VodaBima itawawezesha akina mama na watoto wao kupata huduma za afya ni sehemu ya kampeni inayoendelea ya kampuni hiyo nchini kote ijulikanayo kama ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’.

MWISHO.




Tuesday, 21 November 2023

MSAADA WA KISHERIA WAWAOKOA WATOTO WANAOKINZANA NA SHERIA ZANZIBAR:

Na AMINA MCHEZO:

   Msaada wa watoto kisheria, kisera na kimipango ni uwanja mpana huku ikionekana sheria iliopo Sasa ya mtoto sheria namba 6 ya mwaka 2011 inamapungufu hivyo wizara ya Màendeleo ya jamií, jinsia, wazee na watoto Zanzibar inafanya juhudi kuhakikisha sheria hiyo inapitiwa upya.

   Sheria hiyo Kwa Sasa inaonekana bado haitoi ulinzi Bora Kwa mtoto hivyo Kwa Sasa wadau na taasisi za usimamizi wa mtoto wamekuwa wakiisindikiza tume ya marekebisho ya sheria ili kuwe na sheria mpya.
 
    "Kwa Sasa tumeshatoka kwenye hatua nyingi za ukusanyaji wa maoni ya wadau na Sasa nadhani tupo katika hatua ya kuishirikisha tume ya marekebisho ya sheria ili tuone kwamba tunapata baraka za mwisho na kunipeleka mbele ili tuwe na sheria mpya ili mambo yawe mazur Kwa watoto" Amesema mkuu wa wa Division  ya hifadhi ya mtoto kupitia idara ya ustawi wa jamii na wazee.

   Mtoto anaekinzana na sheria ni mtoto yeyote alie chini ya umri wa miaka 18 ambae amefanya makosa ya kijinai ikiwemo kubaka, kulawiti, wizi na makosa mengine.
 
  Utafiti umebaini kuwa watoto wengi wanaokinzana na Sheria ni wale watoto wa mzazi mmoja, ndoa kuvunjika, Kukosa matunzo Kwa wazazi wake, hivyo watoto hao hupelekea kuathirika kiakili Kwa kujiingiza katika  makundi maovu na kufanya makosa ya kijinai.

   Kiuhalisia kutokana na sababu hizo inaonekana wazi watoto wanaokinzana na sheria wengi wao ni wale waliopitia udhalilishaji Kwa namna Moja au nyengine kutokana na Kukosa malezi sahihi na Kukosa haki zake za msingi kama mtoto.

    Msaada wa kisheria Kwa watoto wanaokinzana na sheria umeibua hisia tofauti Kwa wanajamii hasa pale wanapoona makosa ya namna hiyo yakijirudia Kila mara
     
     Wengine wanasema kupatiwa msaada wa kisheria ni sawa tu kwani wale ni watoto mengi wanayafanya Kwa kutokujua.
   
     Huku mitazamo ya wengine yakionekana kubeba hisia Kali na kukataa kabisa watoto wale kupewa msaada wakidai kuwa ni njia Moja ya watoto hao kuendelea kutenda makosa Kila siku.

     "Sioni sababu ya watoto wanaotenda makosa kupewa msaada wa kisheria  kwani nao wanajielewa na wakisaidiwa  kisheria yaani watoto watakuwa wanajiamini Sana" Wamesema baadhi yao.

      Mtumwa Ameir Ali msaidizi wa sheria kutoka wilaya ya mjini amesema bado baadhi ya  wanajamii hawajaelewa kuhusu kutolewa Kwa msaada wa kisheria Kwa watoto wanaokinzana na sheria.

      Amesema ushawishi wao ni mkubwa Kwa kutafuta wakili wa usimamizi wa kesi za watoto pamoja na wao kumpa elimu na ushauri ili asirudie tena kosa Lile.

     Amefahamisha kuwa kumuacha mtoto aliekinzana na sheria ni kumkosesha haki zake za msingi ikiwemo kusoma pindi tu atakapokaa chuo Cha mafunzo Kwa Kukosa usaidizi wa kisheria.
    
     "Baadhi ya wajamii hawana uwelewa Kwa sababu wanaona yule mtoto ameshatenda Lile kosa kwanini sisi tunakaa tunamtetea lakini jamii hawajui kuwa Lile kosa linaweza kuwa lisiwe lake au amefanya kosa Kwa ule utoto tu." amesema.

     Bi mtumwa amesema ijapokuwa wao sheria inawabana kuingia mahakamani lakini hawawezi kumuacha mtoto aliekinzana na sheria hivyo wanaanza ngazi za awali ikiwemo polisi ili apate haki yake Kwa wepesi na haraka. 

    Jumla ya kesi 129 zimeripotiwa katika mahakama tofauti visiwani Zanzibar kuanzia January Hadi November 2023 zinazowahusu watoto waliokinzana na sheria ,  Kwa mujibu wa kitengo Cha TAKWIMU Dawati la Jinsia Makao Makuu ya polisi Zanzibar.

    Ambapo kesi 70 ni Kwa mkoa wa mjini magharib, 8 mkoa wa kusini unguja, 21 Kwa mkoa wa kaskazini unguja, 16 Kwa mkoa wa kusini Pemba na kesi 14 Kwa mkoa wa kaskazini Pemba.

   Akizungumza na mwandishi wa makala hii mratibu  wa Dawati la  jinsia makao makuu ya polis Zanzibar Sajent Rahma Ali Salum amesema watoto wanaokinzana na sheria wanawaangalia kama watoto wengine hasa katika kuwasaidia Kwa kuwapatia elimu ya kujitambua.

   Amesema  katika usaidizi wao wa kisheria Kwa watoto wa namna hii wanashirikiana na wasaidizi wa sheria, waratibu wa shehia pamoja na ustawi wa jamii  Kwa kusikiliza kesi zao Kwa  pamoja.

     Sagent Rahma amefahamisha kuwa  ni wajibu wa watoto wanaokinzana na sheria kupatiwa msaada kutokana na mazingira yanayojitokeza wakati wanapofanya makosa.

    "Tikifuatilia kesi zao nyingi ni ushawishi wa watoto wezao, wengine kuwa na njaa kutokana na Kukosa chakula nyumbani ilimradi makosa yao mengi ni ya ushawishitu" Amesema Sagent Rahma.

   Amesema Dawati la jinsia wanapopokea kesi za watoto waliotenda makosa wanawaita wazazi wao kuwafahamisha namna ya kukaa na mtoto wake kwani wazazi wengi huwachukia watoto wao kutokana na makosa yao.

   " Msaada wa kisheria Sana wanapewa na wasaidizi wa sheria wanakuwa pamoja na wazazi wao sisi tunawafahamisha namna Yale makosa yalivyo na mtoto akaenae vipi Kwa sababu wazazi wengine  wanakuwa wakali na kimchukia "Amesema.

       Amefahamisha kuwa katika kuwasaidia watoto wamekuwa wakipelekwa katika mahakama ya watoto ili wapate uhuru wa kujieleza mbele ya mahakama.

    Jumuiya ya wanasheria wanawake Zanzibar ZAFELA ni jumuiya isiyo ya kiserikali ambayo inatoa msaada wa kisheria Kwa wanawake na watoto imesema Kuanzia January Hadi November 2023 jumla ya kesi 11 za watoto wanaokinzana na sheria  zimefika ofisini kwao na wameanza  kuzishughulikia Kwa kuwapatia msaada wa kisheria na kesi 3 tayar zimeshapatiwa ufumbuzi Kwa kutozwa faini.

   Mwanaisha Mustapha ni mwanasheria kutoka jumuiya ya wanasheria wanawake Zanzibar ZAFELA amesema Kwa watoto wanaokinzana na sheria wamekuwa wakiwasimamia Kwa hali ya juu kwani wengi wao makosa yao ni ya kusingiziwa au ya kulipiziwa visasi Kwa baadhi ya wanajamii waliomzunguka.

    Amesema wao kama wanasheria wanasimama kwenye sheria ya mtoto inavyozungumza katika kumlinda kama mtoto mwengine mpaka pale mahakama itakapomtia hatiani Kwa kosa Lile.

    Amefahamisha kuwa hali ya Sasa asilimia kubwa watoto Kwa watoto wanafanyiana udhalilishaji jambo ambalo wanataasisi zinazotoa msaada wa kisheria wamekuwa macho ili  jamii ibaki kuwa salama.

   "Ni janga kubwa hali ya udhalilishaji na hali ya Sasa hivi iliokuwepo asilimia kubwa watoto Kwa watoto ndio wengi ambao wanafanya haya matukio Kwa iyo tukiwaangali kisheria wote ni watoto na wote wanataka kulindwa na sheria" Amesema mwanasheria.

    Shirika la msaada wa kisheria nà haki za binaadam  Zanzibar ZALHO kupitia wakili wake bi Jamila massoud  amesema jumla ya kesi 19 wanazishuhulikia katika shirika lao huku kesi 7 zikiwa zimeshafikishwa mahakamani Vuga zinazowahusu watoto wanaokinzana na sheria.

    Amesema  shirika limekuwa na utaratibu wa kuandaa mikutano na wanajamii ili kuzungumza nao na kuwafahamisha kwanini watoto waliokinzana na sheria wanatakiwa kupatiwa msaada wa kisheria.

   Amebainisha kuwa pale wanaposhughulikia kesi za watoto wanaokinzana na sheria wanashauri Sana kubadilishiwa makaazi pale anapokuwa tayar ameshakuwa mtoto mwema kwenye jamii ili asirudia tena makosa yale.

    "Tunawapa muelekeo au tunawapa utaalamu kwanini tunawasaidia hawa watoto Kwa sababu hawa ni Victim wa udhalilishaji ukiangalia mtoto anaekinzana na sheria utagundua kuwa nae kadhalilishwa Kwa namna Moja au nyengine" Amesema.

      Mohd Khamis Faki mkaazi wa kazole anaemlea mtoto wa dada yake  ajulikanae Kwa jina Khamis Mwadini Kheir mwenye umri wa  miaka 16 alishtumiwa Kwa kosa la kukashifu mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 16 mnamo mwezi wa march 2023 huko maeneo ya Daraja bovu wilaya ya maghari A unguja.

     Katika shtaka Hilo lililopekea kufikishwa kituo Cha polisi Mwera na kesi kupelekwa mahakamani Vuga mjini unguja, ndugu Mohd Khamis amesema baada ya kufikishwa mahakamani shtaka la mjomba wake awali walishindwa Kwa Kukosa wakili kutokana na hali yao ya kimaisha.

      "Tulipandishwa mahakamani Vuga tulishindwa kupata wakili kutokana na hali zetu ndipo tukaunganishwa na Mtu kwenye hili shirika hili pale mikunguni linalosaidia watu wasio na uwezo na Kwa uwezo wa Mwnyezi Mungu Lile shirika lilitusaidia mpaka kesi ilipomalizika na alhamdullillah hatukutozwa  ushuru wowote ule" Ameongeza

      Amesema msaada walioupata kutoka shirika la ZALHO ni mkubwa kwani walishindwa na fedha za kuwapa wakili ili kuwasaidia kesi ya mjomba wake na Kwa Sasa mjomba wake huyo yupo huru na amejifunza kutokana na kosa Lile pamoja na kimkataza kufika katika mtaa aliopatia mtihani huo.

     "Kwa Sasa tumempiga Marufuku kufika mitaa ya Daraja bovu ambako ndipo alipo huyo binty kwenye hiyo nyumba aliofika mjomba wangu na Kwa Sasa hata hasogei kwani ulikuwa ni mtihani tu ule kwake" Amesema.

    Wizara ya Màendeleo ya jamií, jinsia wazee na watoto Zanzibar imesema hali ya upatikanaji huduma kisheria Kwa watoto ni ndogo na ndio maana wameona Kuna haja ya kutia mkono sheria iliopo Sasa ili kuboreshwa Kwa huduma.

   Mkuu wa Division ya hifadhi ya mtoto idara ya ustawi wa jamii na wazee ndugu sheikh Ali Sheikh amesema watoto wanaokizana na sheria sheria bado inamtanzama kama mtoto mbali ya kuwa wanatenda makosa lakini sheria inataka kuwalinda pia na kupewa haki zao.

   Amesema kama idara inatoa msaada wa kisheria Kwa kuwasimamia mahakamani hadi pale hukumu zinapotokea ambazo kikawaida ni kutozwa faini tu na sio kufungwa baadae idara inawapeleka vituo vya kurekebisha tabia kwenda kupata ujunzi na kujiweka sawa.

   "Tunamsaidia kama mtoto kama sheria inavyotaka atizamwe Kwa hiyo Kuna maafisa wetu mahakamani kuhakikisha juu ya kesi zao kama watenda makosa lakini mwisho wa siku Sheria inataka iwalinde" amesema.

    Kwa mujibu wa Wizara husika, taasisi za usaidizi wa sheria, waratibu na wadau mbali mbali mbali, suala la usaidizi wa sheria linahitaji kupewa kipaumbele Zaid huku wazazi nao wakitakiwa kusimamia msingi mzima wa malezi Kwa watoto wao ili kupatikana kizazi chenye maadili mazuri.

MWISHO..........0772694778





Tuesday, 17 October 2023

WADAU WA KUPINGA VITENDO VYA UDHALILISHAJI WAIJADILI SHERIA YA MTOTO NAMBARI 6 YA MWAKA 2011



Na Yassir Mkubwa EL BAHSAANY

Wadau wa kupinga Vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji wa kijinsia wamesema Sheria ya Mtoto namba 6 ya mwaka 2011 ni vyema ikatambua mgawanyo  wa haki za watoto kwa kuzingatia umri ili kulinda maslahi na ustawi wa mtoto.

Wito huo umetolewa na na Hakimu dhamana Mkoa wa Kusini Unguja ndugu Khamis Rashid Khamis  Mara baada ya kikao  cha Mapitio cha  kujadili  sheria ya Mtoto na kutoa maoni kilichofanyika katika ukumbi wa kidongo chekundu Mental.

Amesema ni wakati sahihi  wa kueka sheria ambayo Itatoa muongozo wa kushughulikia watoto wenye umri wa chini ya miaka 14  na 16 na kuweka utaratibu wa kusikiliza kesi zao.





Hata hivyo amependekeza  suala la kueka sheria kwa skuli zinazolea watoto kuhakisha wanaimarisha mfumo wa kuieka saikolijia ya mtoto mhanga wa matukio mbali mbali nchini.

Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee  na Watoto ndugu Siti Abas Ali amesema umuhimu wa marekebisho ya Sheria ya  mtoto ni pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia  ambayo kimsingi yameongeza haja ya kuimarisha baadhi ya vipengele vyake.

Aidha Mkurugenzi Siti amesisitiza suala la ushirikiano na wadau mbali mbali katika katika mapambano ya ukiukwaji wa haki za mtoto.

Amesema Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ipo tayari kushirikiana  na wadau hao  ili kufanikisha azma ya kuleta ustawi wa mtoto.

Baadhi ya wanasheria wamesema kikao hicho ni miongoni mwa sheria yoyote ni kutekeleza hivyo uwepo wa Ushirikishwaji wa wadau hao utasaidia kuleta ufanisi wa kiutekekelezaji wa sheria hiyo.

Wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia Wazee na watoto inaendelea na ukusanyaji wa maoni ya sheria ya hiyo kwa lengo la kuipata sheria mpya na iweze kudumu kwa muda mrefu.

MWISHO

Tuesday, 8 August 2023

WAHANDISHI WANAWAKE WANAMCHANGO MKUBWA KATIKA KULETA UCHUMI WA MAENDELEO YA NCHI - DKT MWINYI

NA MUANDISHI WETU


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ametoa wito kwa Wahandisi wanawake kushirikiana na kuhakikisha wanachangia vilivyo maendeleo ya nchi kufikia malengo ya kuwa na uchumi wa juu na wa kati ifikapo mwaka 2025.


Dk. Mwinyi alitoa wito huo kwenye ufunguzi wa Kongamano la nane la Wahandisi wanawake, ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege, Mkoa wa Mjini Magharibi.


Alisema, Serikali za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar, zinatambua na kuthamini mchango wa Wahandisi wanawake nchini kutokana na kazi za uhandisi wanazozifanya.


Alisema, Makangamano kama hayo yamekuwa na mchango mkubwa wa kuunga mkono juhudi za Serikali za kuendeleza ubunifu wa sanyansi na kuleta chachu ya maendeleo ya Taifa ikiwemo ujenzi wa viwanda, uboreshwaji miondombinu, utumiaji mzuri wa rasilimali na malighafi, usafiri na mawasiliano.


Dk. Mwinyi aliongeza, Serikali zote mbili zinajitahidi kushirikisha wanawake kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo kwa kuwawekea mazingira wezeshi ya kujiajiri, kuhamasisha utambuzi wa fursa mbalimbali kupitia rasilimali zilizopo nchini, kurejesha stadi za ujuzi, elimu ya uanagenzi vyuoni na kutenga bajeti kwa ajili ya kufanikisha shughuli za utafiti na ubunifu wa fani tofauti.


Alisema, fani ya uhandisi ina umuhimu mkubwa kwa ustawi wa nchi pia ni uti wa mgongo wa shughuli nyingi za kiuchumi. Hivyo aliwataka vijana na wanawake kuzitumia fursa ziliopo ili kuyafikia malengo yao.


Pia, aliwashauri wahandisi wanawake kufungua kampuni na kujiajiri kupitia ukandarasi na uhandisi nakueleza hatua hiyo itachangia sana maendeleo ya nchi kwa kujenga miundombinu imara itakayodumu kwa muda uliokusudiwa.


Aidha, alieleza kutokana na idadi ndogo ya wahandisi iliopo nchini, Serikali za SMZ na SMT zinaendelea kuweka mipango madhubuti ya kuongeza idadi ya wahandisi wanawake na mafundi sanifu pamoja na kuhakikisha wanasaidiwa vizuri wasichana wanaosoma masomo ya Sayansi katika elimu za Sekondari, vyuo vya mafunzo ya amali na vyuo vikuu, hatua ambayo bila shaka itasaidia kuongeza idadi ya wahandisi wanawake nchini.  

 

Hata hivyo, alihimiza ushirikiano baina ya wahandisi wanawake wa Zanzibar na Kitengo cha Taasisi ya Wahandisi Tanzania Bara kwa madhumuni ya kuendeleza sekta ya uhandisi nchini Tanzania.


Akizungumza kwenye kongamano hilo kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Mhandisi Aisha Amour alisema Serikali inatambua mchango wa wahandisi katika kukuza uchumi wa taifa  uanzishwaji wa viwanda mbalimbali.


Naye, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Dk. Khalid Salum Muhamed alieleza kongamano la nane la wahandisi wanawake linaloendelea visiwani Zanzibar litaongeza hamasa na uelewa kwa vijana na kuwashajihisha zaidi wanafunzi kuendelea kupenda masomo ya sayansi ili kujijengea kada zenye tija na utaalamu, kwani bado mahitaji ya wahandisi wanawake bara na Zanzibar yanahitajika.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa taasisi ya wahandisi Tanzania, kitengo cha wanawake, Rihanna Juma aliisihi jamii kuachana na mitazamo potofu juu ya wahandisi wanawake kwa kuangalia mapungufu yao yanayotokana maumbile ya jinsia zao zikiwemo uzazi na uhalisia wao, hivyo aliwataka waajiri kuona umuhimu wao na kutambua mchango wao kwa maendeleo ya taifa kwa kuwatumia kwenye kazi za vitendo badala ya kuwapa kazi za ofisini pekee.


Uzinduzi wa Kongamano la nane la wanahandisi wanawake Tanzania kwa mwaka huu, 2023 ulikwenda sambamba kaulimbiu isemayo “Nguvu ya Ushirikishwaji na Uhusishwaji wa Wanawake katika kazi za Kihandisi” 

MWISHO.





Thursday, 20 July 2023

FURAHA YA WATOTO IMEONGEZEKA KWA KUPEWA MIKOBA RC AYOUB ASHUHUDIA

 Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud amesema serikali inaendelea kushirikiana na sekta binafsi ili kuona changamoto zinazozikabili sekta mbalimbali ikiwemo elimu zinapatiwa ufumbuzi.

 Akizungumza katika hafla ya ugawaji wa vifaa  vya elimu kwa wanafunzi wa skuli ya Mgonjoni  vilivyotolewa naTaasisi ya Bhoke Moren Foundation  amesema kutolewa kwa vifaa hivyo vitawasaidia wanafunzi hao kusoma katika mazingira mazuri.

 Amesema matumaini yake kuwa taasisi hiyo inakuwa mkombozi wa wanafunzi ktk sekta ya elimu hapa zanzibar .Amesema serikali imefanya juhudi za kutosha kuhakikisha kijiji cha mgonjon kinapata mafanikio pamoja na kupatiwa huduma zote za msingi ikiwemo elimu na huduma nyengine za kijamii.

 Mwenyekiti wa Bhoke Moroni Foundation Bhoke Moroni amesema taasisi ya Bhoke amelenga kusaidia watoto wenye kuishi katika mazingira magumu hivyo atahakikisha misaada yote inayotolewa inawafikia walengwa ili kuwaondolea changamoto mbalimbali ikiwemo kwenye elimu. Ameeleza lengo ni kuinua ufaulu wa wanafunzi wenye kuishi katika mazingira magumu wakiwemo watoto yatima amesema katika kuangalia mazingira wamegundua mazingira hatarisi ikiwemo viatu na sare za skuli.

Ameahidi kuwapatia wanafunzi viatu na sare za skuli ili kuondoa tatizo hilo ambalo wanafunzi wengi wanakabiliwa nalo kutokana na ugumu wa maisha katika familia zao.

Akisoma Risala ya walimu ya Skuli ya Mgongoni Mwalimu Zainab Sururu Vuai amesema Skuli ya Mgonjon bado inakabiliwa na changamoto  ya Uzio wa skuli, Usafiri kwa walimu, ukosefu wa uwanja wa michezo, walimu wa masomo ya Sayansi komputa na ICT.Hivyo ameiyomba serikali kupitia wizara ya elimu kuongeza bajeti ili kujiendesha kwa ufanisi katika kukuza ufaulu kwa wanafunzi wa skuli hiyo. 

Hata hivyo waliishukuru taasisi ya msaada Bhoke Moroni Foundation kwa kuwapatia msaada hu wa vifaa na kuahidi  kuvitumia kwa lengo lililokusudiwa na taaasisi hiyo. Nao wanafunzi waliokabidhiwa msaada huo wamatoa shukurani zao za dhati kwa taasisi ya Bhoke ambao utawasaidia katika masomo yao. 


Tuesday, 18 July 2023

DKT MWINYI MGENI RASMIN KILELE CHA MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA KIISLAMU PEMBA

 DK. MWINYI AKAMILISHA ZIARA YAKE PEMBA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al hajj. Dk. Hussein Ali Mwinyi amehimiza jamii kuweka mkazo zaidi kwenye malezi ya watoto na vijana ili kukuza taifa lenye maadili, nidhamu na kizazi chema chenye kumjua Mwenyezi Mungu.

Al hajj Dk. Mwinyi aliyasema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya Mwaka mpaya wa Kiislam Zanzibar, 1445 Hijria, masjid  Munawwara, Mfikiwa  Mkoa wa Kusini, Pemba.

Alisema, ni wajibu wa wazazi na walezi kuwasimamia vyema watoto wao na kuwapa elimu ya dini na dunia ili kuwaepusha na vitendo vya uvunjivu wa amani, tabia mbaya na vitendo vya udhalilishaji.

Akizungumzia historia ya tarehe ya Kiislaam, Al hajj Dk. Mwinyi alieleza ilianza mara baada ya  Mtume SAW kuhama Makka na kuhamia Madina ambako utulivu na Amani ulipatikana na kuwa chanzo cha kuenea uislam dunia nzima.

Alisema lengo la kuadhimishwa mwaka Mpya wa Kiislam 1445 H ni kuendelea kusisitiza na kuhimiza amani, ushirikiano na upendo kwenye jamii Katika kutekeleza mambo ya heri.

Aidha, aliendelea kuhimiza Umoja na mshikamano kwenye jamii ili nchi izidi kupata neema na baraka kutoka kwa Mola.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haroon Ali Suleiman, alipongeza ushirikiano uliopo baina viongozi wa Mkoa wa Kusini na Kaskazini Pemba na viongozi wa Chama, katika kutela Maendeleo ya kisiwa hicho.

Akiwasilisha mada nidhamu ya kodi kwenye kongamano la mwaka mpya wa kiislaam 1445, Sheikh Said Ahmad aliwataka watumishi wa Umma kuutumia vyema muda wa Serikali wanapokua kwenye majukumu yao ili kukwepa kuchuma mali za dhulma zinazotokana na utumishi waa hasa kwenye ibada zao.

Pia alihimiza umuhimu wa kulipa Kodi kwa  serikali kwa mujibu wa sheria za Kiislam.

 Naye Sheikh  Izud Alaw wa Mombasa Kenya,  aliwahimiza waumini wa Kiislam juu ya umuhimu wa kuzingatia vyema tarehe za kiislam kwenye mfumo wa maisha yao.

Pia alieza miezi ya Kiislaam inabeba mfumo mzima wa  maisha ya binaadam.

Vile vile, aliwataka waumini wa dini ya Kiislaam kutofungamana na kufuatilia masuala na muandamo wa mwenzi na hitilafu za Arafa pekee pia waangalie mambo mengine muhimu ikiwemo suala la eda kwa mwanamke alieacha ama kufiliwa na mumewe kwa tarehe zinapoanza hadi kumalizika kwake.

Akiwasilisha taarifa ya maadhimisho ya mwaka mpya wa Kiislam 1445, Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti , Sheikh Khalid Mfaume, alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuitangaza tarehe ya kiislam na kuendeleza historia ya dini walioiacha maulamaa na kuahidi ofisi ya Mufti inajukimu ya kuendelea kuitangaza na kuishajisha kwa jamii.

Alisema maadhimisho ya mwaka mpya wa Kiislam yalifanikishwa kwa matukio mbalimbali ikiwemo kutoa huduma za macho kwenye hospitali ya kivunge, Mkoa wa Kaskazini Unguja, kusomwa dua ya kuliombea Taifa, kufanikishwa kwa kongamano kuwa la wanawake wa Kiislam lililohudhuriwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Hajjat Dk. Samia Suluhu Hassan, maonesho ya kiislam ya biashara yaliyowashirikisha wafanyabiasha wadogo na wajasiriamali, matembezi ya Zafa, kisiwani Pemba  yaliolenga kuboresha afya pamoja na matembezi ya hiari yatafanyika Unguja.

MWISHO.




MAHAKAMA YAMUACHIA HURU AFANDE RAMA

 NA YASSIR MKUBWA EL BAHSAANY

MAHAKAMA YAMUACHIA HURU AFANDE RAMA

Mahkama ya Mkoa wa Vuga mjini Unguja  imemuachua huru mshtakiwa Ramadha Ali ( Afande Rama) aliekua kikabiliwa na kosa la kuruhusu kuingiliwa kuingiliwa.

Mshtakiwa  mwenye kesi namba 59/ 2023 leo ameachiwa huru baada ya hakimu wa mahakama hiyo kudai mshatakiwa hana hatia.

Akitoa hukumu ya kumuachia huru hakimu wa mahakama ya hiyo  Mhe Khamis Ali Simai amesema mshitakiwa hana hatia hvyo amemuachia huru kwa kifungu cha 220 sheria namba 7 ya mwaka 2018.

Kesi hiyo imewasilishwa na muendesha mashitaka kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka Mohd Saleh Jumla ya mashahidi 9 wamewasilisha ushahidi ambao ushahidi wote haukuweza kumtia hatiani mshtakiwa huyo.

Itakumbukwa kuwa Ramadhani alishatakiwa baada ya kusambaa kwa video zilizodhaniwa kuwa ni yeye ambae aliruhusu kuingiliwa wakati akiwa mtumishi wa jeshi la Polisi.

MWISHO.


Tuesday, 9 May 2023

ZAIDI YA MITI 5000 YA ASILI NA MATUNDA INATARAJIWA KUPANDWA MATEMWE

NA THABIT MADAI, ZANZIBAR 

KATIKA Kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Tabia Nchi, Jumla ya Miti 5000 inatarajiwa kupandwa katika Kijiji cha Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja kupitia Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mfumo wa Ikolojia Vijijini (EBARR).

Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mfumo wa Ikolojia Vijijini unatekelezwa katika ya Simanjiro, Mpwapwa,Mvomero, kishapu na Wilaya ya Kaskazini A Unguja.

Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari huko Maruhubi Mjini Magharib Unguja, Mratibu wa Mradi wa EBARR  wa Zanzibar, Alawi Haji Hija, alisema kuwa lengo la upandaji wa Miti hiyo ya Asili na Matunda ni lengo la kuhimili mabadilko ya tabianchi na kurejesha uoto asili na matumizi bora ya ardhi.

Pia alisema, kupitia mradi huo pia watajenga vitalu nyumba ambapo ni kilimo kimekuwa kikistahamili ukame.

Alisema,mradi huo kwa upande wa Zanzibar wanatekeleza kwa shehia tatu zilizoko katika kijiji cha Matemwe, ikiwemo shehia ya Matembe kijini, Matemwe mbuyu tende na shehia ya Matemwe Jugakuu.

Alisema, lengo la mradi huo ni kuimarisha uoto wa asili kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi, ambapo alisema athari hizo zipo katika maeneo mbalimbali na kila eneo limekuwa na athari zake.

“Kwa upande wa matemwe ni maeneo ambayo yameathirika na kunatatizo kubwa la ukosefu wa mvua za kutosha na ukiangalia katika mazingira ya eneo lile kuna uharibifu mkubwa wa misitu” alisema.

Hivyo, alisema wataendeleo kurejesha hali hiyo sambamba na kuwapatia kipato wananchi kwa kuwawezesha kupata kipato chao bila ya hata kuharibu mazingira.

Hivyo, alisema mradi huo umekuwa unawasaidia wanajamii hata kupata kipato na kuwahimiza shughuli zao zisiwe moja kwa moja atika shughuli za kuharribu mazingira.

Alisema ili kudhibiti suala hilo, wamegenga majiko banifu ambapo yamekuwa yakitumia kuni chache kwa muda mrefu, jambo ambalo limekuwa likiwapa afueni miti iliyozunguka katika eneo hilo.

Aidha alisema pia kupitia mradi huo wamechimba visima sita vimechimbwa ili kuwezesha upatikanaji wa maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kilimo cha mbogamboga, wameviwezesha vikundi vya uvuvi kwa kuwanunulia boti sita za kisasa.

Nao, waandishi wa habari, wamesema watendelea kushirikiana na watendaji wa mradi huo ili kuona hali ya tabiachi inaendelea kuimarika sambamba na kuahidi kutoa elimu kwa jamii ili kuondokana na uharibifu wa mazingira.

Mradi wa EBARR unatekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Shirika La Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP)ambapo utekelezaji huo ulianza mwaka 2018 na unategemewa kukamilika Februari  2024.

MWISHO.



Wednesday, 3 May 2023

UHURU WA HABARI UTUMIKE KATIKA KUJIELEZA

Na Muandishi Wetu 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa wito kwa tasnia ya habari kuitumia fursa ya maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kuweka mkazo mkubwa kwenye uhuru wa kujieleza ndani ya ajenda ya jumla ya haki za binaadamu, kwa kuangazia uhusiano baina ya uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza na haki nyengine.

Aidha, aliwaasa waandishi wa Habari kushirikisha wahusika wote kwa madhumuni ya kulinda uhuru wa vyombo hivyo, kuimarisha uhuru wa kujieleza, na kuweka mazingatio ya haki za binaadamu kama ni kitovu cha kufanya maamuzi katika ngazi ya kimataifa, kikanda na kitaifa.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani huko ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa ndege, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Katika maadhimisho hayo, Rais Dk. Mwinyi pia aliwataka waandishi wa habari kutimiza ahadi zilizotolewa na kila nchi Mwanachama wa Umoja wa Mataifa ili kuyafikia malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).

Pia Dk. Mwinyi aliwataka wadau wa vyombo vya habari kuitumia siku hiyo kusherehekea kwa kuungana na mashirika yanayotangaza masuala ya mazingira, haki za wanawake, watoto, haki za kiasili, haki za kidijitali, vita dhidi ya ufisadi na mengineyo.

Alisema, maadhimisho hayo ni jukwaa muhimu katika kuibua changamoto za kisera na kuangalia namna bora ya kuboresha mazingira ya kuendesha vyombo vya habari nchini.

Akizungumzia sheria ya Habari, Rais Dk. Mwinyi alisema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari imeandaa mswada wa sheria hiyo yenye madhumuni ya kufuta Sheria iliyopo ya Usajili wa Magazeti, Wakala wa Habari na vitabu Sheiria nambari 5 ya mwaka 1988 ambapo marekebisho yake ni sheria nambari 8 ya mwaka 1997 na kutunga Sheria mpya ya Huduma za Habari na Mambo yanayohusiana na hayo.

Dk. Mwinyi alieleza kwamba Mswada huo tayari uko Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na unatarajiwa kutoa sheria nzuri itakayohusiana na masuala ya habari.

Alisema Zanzibar, imekuwa na kasi ya usajili mpya wa vyombo vya habari hasa vya kielektroniki kupitia Tume ya Utangazaji baina yam waka 2020 hadi 2023. Kwa mijibu wa tume hiyo Dk. Mwinyi alieleza jumla ya TV 21 za kawaida na 38 za mitandaoni zimesajiliwa, jumla ya redio 27 zikiwemo za masafa ya FM na za jamii zimesajiliwa. 

Aidha, alizungummzia Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, magazeti na majarida 71 yamesajiliwa tangu mwaka 1998 hadi 2023. Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) na Shirika la Magazeti ya Serikali ni vyombo vya habari vya Serikali ambavyo navyo vimekuwa vikifanya kazi kubwa za kutoa taarifa kwa umma.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Andrew Kundo, aliviasa vyombo vya Habari nchini kufanyakazi kwa kuzingatia, miongozo, kanuni na sheria zilipo katika utekelezaji wa majukumu yao.

Naye, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita, alisema Serikali kupitia Wizara ya Habari itaendelea kushirikiana na wadau wa vyombo vya Habari nchini ili kuendelea kuwapasha habari wananchi.

Mkurugenzi kutoka Chama Cha Waandishi wa Habari wanawake Tanzania, TAMWA, Joyce Shebe aliomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuharakisha mchakato wa Sheria ya Habari.

Jumla ya magazeti 312 yalisajiliwa nchini hadi tarehe 20 Februari, mwaka huu, ambapo baada ya Uhuru wa Tanganyika, kulikuwa na magezeti 10 tu.

Kwamujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) hadi mwezi Februari mwaka huu, jumla ya redio 218, televisheni 68, redio za mtandao nane, televisheni za mtandao 391, blog, majukwaa 73 na cable operators 53 zimesajiliwa Tanzania bara, ambapo taarifa za baada ya uhuru zinaonyesha tulikuwa na kituo kimoja tu cha redio cha Tanganyika na hakukuwa na kituo cha televisheni hata kimoja, blogs wala majukwaa ya mtandaoni.




UJENZI WA VITUO VYA MABASI KUTAONDOSHA CHANGAMOTO KWA WANANCHI

 UJENZI WA VITUO VYA MABASI KUTAONDOSHA CHANGAMOTO KWA WANANCHI

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dk. Khalid Salum Mohamed ameitaka kampuni ya CRJE Tanzania iliopewa kazi ya kujenga kituo cha mabasi katika eneo la kijangwani kuhakikisha wanazingatia viwango na kukamilisha mradi huo ndani ya wakati uliopangwa.

Waziri Dk. Khalid ametoa agizo hilo wakati aliposhiriki na kushuhudia zoezi la utiaji saini wa ujenzi wa kituo hicho hafla iliofanyika katika ukumbi wa ZSSF Kariakoo.

Zoezi la utiaji saini kwa upande wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF) imewakilishwa na Mkurugenzi Muendeshaji wa Mfuko huo ndugu Nassor Shaaban Ameir na kwa upande wa Kampuni ya CRJE imewakilishwa na meneja wao XU CHANG.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi la utiaji saini Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dk. Khalid Salum Mohamed ameupongeza uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF) kwa uthubutu pamoja na ubunifu wao wa kutekeleza miradi ya maendeleo.

Aidha, Mhe. Waziri ameutaka uongozi wa ZSSF kuhakikisha wanasimamia kwa karibu ujenzi wa kituo hicho kwa kuteua mshauri elekezi ataekasimamia kwa upande wa Serikali na kuhakikisha ujenzi huo unakamilishwa kwa viwango vinavotakiwa.

Pamoja na mambo mengine Waziri Dk. Khalid amesema ZSSF inakwenda kurejesha historia kwa kukijenga kituo cha mabasi katika eneo hilo kwani mnamo miaka ya 1970 eneo hilo lilikua likitumiwa kwa shughuli kama hizo.

Pia, Mhe. Waziri amepongeza ushirikiano mzuri ulitolewa na askari wa UMAWA kwa kukubali kupisha ujenzi wa kituo hicho na kuhamishia Afisi zao katika eneo jengine lililotolewa na Serikali.

Nae Mkurugenzi Muendeshaji wa mfuko wa Hifadhi ya Jamii Ndugu Nassor Shaaban Ameir amesema ZSSF imeamua kujikita katika ujenzi wa vituo vitatu vya mabasi kwa hatua ya awali lengo likiwa ni kutatua changamoto na kuwaondoshea usumbufu wananchi katika huduma ya usafiri.

Amebainisha vituo hivyo vitajengwa katika eneo la Kijangwani, Malindi pamoja na katika eneo la Mnazi mmoja huku wakisogeza huduma ya ujenzi wa vituo hivyo nje ya mji kulingana na uhitaji.

Vile vile Mkurugenzi Nassor amemuomba Mhe. Waziri kupitia wizara anayoisimamia kuziagiza mamlaka za usafiri pamoja na mabaraza ya manispaa na mabaraza ya miji kuanza kutunga kanuni na kuandaa utaratibu wa kutumika kwa vituo hivyo mara vitakapokamilika.

Kwa upande wake Meneja wa kampuni ya CRJE Tanzania XU CHANG ameeleza kwamba, kampuni yao itahakikisha inajenga kituo hicho katika ubora unaotakiwa na kumaliza kwa wakati uliopangwa ambapo wanakusudia kuingiza vifaa vya ujenzi vya kisasa katika kutekeleza kazi hiyo ya ujenzi.

Ujenzi wa Kituo hicho unatarajiwa kugharimu jumla ya Shilling Billlioni nane milioni mia sita nasabiini, laki nne na arubaini na tisa mia tatu ishirini na moja nukata mbili moja (8,670,449,321.21) na kinakadiriwa kuwa na maduka sabiini na nane (78), sehemu za kupata huduma kutolea fedha sita, sehemu za kutoa huduma za chakula tano pamoja na huduma za vyoo ambapo ujenzi wake utachukua miezi kumi (10) hadi kukamilika kwake. 




Monday, 1 May 2023

WANNE MIKONONI MWA POLISI KWA WIZI WA HONDA

 NA MUANDISHI WETU - ZANZIBAR

JESHI LA POLISI MKOA WA KUSINI UNGUJA LIMEWAKAMATA WATU WANNE

WAKIWA NA PIKIPIKI MBILI ZINAZODAIWA KUWA NI ZA WIZI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA KUSINI UNGUJA, KAMISHNA MSAIDIZI WA

POLISI ACP GAUDIANUS KAMUGISHA AMEWATAJA WATUHUMIWA HAO KUWA NI

MOSES EDWIN ENDRU MIAKA 28 NA AHMADA MSHAMBA MUSSA MIAKA 27

WOTE WAKAAZI WA MWERA, WILAYA YA MAGHARIBI ”A” WAMEPATIKANA

WAKIWA NA PIKIPIKI MOJA AINA YA TVS RANGI NYEUSI YENYE NAMBA ZA USAJILI

Z.944 KU AMBAYO INADAIWA KUIBIWA MAENEO YA TUNGUU.

AIDHA KAMANDA KAMUGISHA AMEWATAJA ABDUL-RAHMAN SULEIMAN SAID

MIAKA 32 NA ALI ABDALLAH ABDALLAH MIAKA 48 WOTE WAKAAZI MIGOMBANI

MJINI UNGUJA WAKIWA NA PIKIPIKI MOJA RANGI NYEUSI AINA YA TVS YENYE

NAMBA ZA USAJILI MC.884 CKZ.